Skip to content
Media

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: Chuo Kikuu cha Columbia Chatangaza Ushirikiano na Hifadhi ya Nyaraka za Kidijitali za Salim Ahmed Salim

  • Share

Chuo Kikuu cha Columbia Chatangaza Ushirikiano na Hifadhi ya Nyaraka za Kidijitali za Salim Ahmed Salim

Dar es Salaam/Nairobi: Kituo cha Kimataifa cha Chuo Kikuu cha Columbia Nairobi (CGC Nairobi), kituo kinachokuza na kuwezesha ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Columbia na dunia, kimetangaza ushirikiano wa kihistoria na Hifadhi ya Nyaraka za Kidijitali za Salim Ahmed Salim (SAS Digital Archive). Ushirikiano huo utajumuisha mfululizo wa kipekee (webinars) unaochunguza maisha na urithi wa Dkt. Salim na kutoa mafunzo kutoka kwenye hifadhi kwa kushirikiana na kundi la wasomi mashuhuri, wanadiplomasia na wataalamu.

Dkt. Salim ni mhitimu wa Shule ya Masuala ya Kimataifa na Umma kutoka Chuo Kikuu cha Columbia, ambako alihudumu kama Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa huku akiendelea na masomo yake. Ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Columbia na Hifadhi ya Nyaraka za Kidijitali za SAS utakaribisha mazungumzo yanayochochea suala la uongozi bora ili kuharakisha maendeleo barani Afrika kwa kutumia maarifa wa kihistoria yaliyopo kwenye Hifadhi ya Nyaraka kuhusu siasa za kimataifa katika muktadha wa Afrika kwa kipindi cha miongo sita.

Akizungumzia ushirikiano huo, Dkt. Murugi Ndirangu, Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Columbia jijini Nairobi alisema:

“Ahadi ya Afrika iliyochangamka zaidi na inayokuwa kwa kasi zaidi iko kwenye kukuza maadili bora ya uongozi. Maadili haya yanapaswa kuwekwa kipaumbele, sio tu maendeleo ya kiuchumi bali pia heshima na uwezeshaji wa watu wa Afrika. Dkt. Salim, rafiki wa karibu wa CGC | Nairobi, ni mfano wa kanuni hizi na anatutia moyo kujivunia kuwakilisha roho ya Kiafrika katika jukwaa la kimataifa.”

CGC | Nairobi itachambua hadithi na masimulizi mbalimbali yaliyopo kwenye Hifadhi ya Nyaraka ikishirikiana na kundi maalum la wataalamu, wanadiplomasia na wasomi. Lengo la CGC|Nairobi la kuhamasisha jamii kwa kupitia utafiti, mazungumzo na utendaji inaendana na malengo ya Hifadhi ya Nyaraka za Kidijitali ya SAS. Mfululizo huu utahusisha mijadala kuhusu uongozi, utawala, masuala ya kidijitali na upatikanaji wa habari.

Kikao cha kwanza kitafanyika Julai 18 saa kumi jioni kwa saa za Afrika Mashariki na kitaangalia sanaa ya kusimamia uongozi bora katika ulimwengu unaozidi kuwa tete.

Hifadhi-ya-Nyaraka-za-SAS-Chuo-Kikuu-cha-Columbia-Taarifa-kwa-Vyombo-vya-Habari-Julai-2024.pdf

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: Chuo Kikuu cha Columbia Chatangaza Ushirikiano na Hifadhi ya Nyaraka za Kidijitali za Salim Ahmed Salim

Hifadhi-ya-Nyaraka-za-SAS-Chuo-Kikuu-cha-Columbia-Taarifa-kwa-Vyombo-vya-Habari-Julai-2024.pdf
553 KB
Go to external page: Download