Hotuba Ya Kukubali Uteuzi Na Kusimikwa Kwakwe Kuwa Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Kumbukumbu Ya Hubert Kairuki
"Kusema kweli, ilinibidi kufikiria sana kabla ya kukubali ombi la Bodi ya Wadhamini la kuwa Mkuu wa Chuo wa Pili wa Chuo Kikuu hiki. Kusita kwangu kwa mwanzo, hakuhusiani na tathmini yangu kuhusu umuhimu na faida za asasi hii ya elimu ya juu, kwa kuwa umuhimu huu ni jambo pla dhahiri. Bali, ni kutokana na mimi mwenyewe kuitambua mipaka yangu na nilitaka kujihakikishia mwenyewe kama nitaweza kuwa wa msaada kwa Chuo Kikuu hiki.
Lakini wasiwasi wowote ule niliokuwa nao, uliondolewa na mambo makuu wawili ya msingi. Kwanza, nimetiwa moyo na dira na kujitoa kwa dhati kwa Mkuu wa Chuo mwanzilishi, ambaye pamoja na majukumu yake mengi ya kitaifa, alikubali kuwa Mkuu wa Chuo. Vilevile, nilivutiwa sana na dira pamoja na michango ya Mwanzilishi na Makamu wa Mkuu wa Chuo. Watanzania hawa wawili maarufu waliotutoka, Marehemu Dkt. Omar All Juma na Marehemu Profesa Hubert Kairuki, wameweka mfano kwa jinsi walivyoupa umuhimu maendeleo na uendeleza].i wa elimu ya juu katika jamii yetu." - Dr. Salim, November 1, 2003